31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DAKTARI AKWAMISHA KESI YA SCORPION

IMG_1756

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

USHAHIDI katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi  inayomkabili, Salum Njwete (34) maarufu Scorpion, umeshindwa kuendelea baada ya upande wa Jamhuri kudai shahidi  hakufika.

Sababu za kutofika kwa shahidi huyo ambaye  ni  daktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ni kutokana na kuwa nje ya kituo chake cha kazi hivyo hakupatikana   jana.

Mshitakiwa Scorpion alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi upande wa Jamhuri.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai upande wa Jamhuri ulipanga kumhoji  shahidi ambaye ni daktari lakini kwa vile alikuwa  na dharura ingefaa mahakama impangie tarehe nyingine.

“Mheshimiwa hakimu shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na upande wa Jamhuri ulipanga kumleta shahidi ambaye ni daktari lakini ameshindwa kufika leo, ana dharura ambayo inaweza ikachukua wiki tatu.

“Hivyo kwa mujibu wa kifungu namba 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi ya Makosa ya Jinai ambayo inataka kesi isiahirishwe zaidi ya wiki mbili kama mshitakiwa yuko mahabusu,   tunaomba mahakama itaje hapa  tupange tarehe ya kusikilizwa,’’alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles