27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA ‘PEDESHEE NDAMA’ YAPIGWA KALENDA  

Na PATRICIA KIMELEMETA- DAR ES SALAAM


 

Mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, Ndama Shaaban Hussein, maarufu ‘Pedeshee Ndama Mtoto ya Ng’ombe’ (katikati), akiwa chini ya ulinzi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana alipofikishwa kwa kesi mbalimbali  zinazomkabili, ikiwamo ya utakatishaji fedha. Na Mpigapicha Wetu
Mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, Ndama Shaaban Hussein, maarufu ‘Pedeshee Ndama Mtoto ya Ng’ombe’ (katikati), akiwa chini ya ulinzi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana alipofikishwa kwa kesi mbalimbali zinazomkabili, ikiwamo ya utakatishaji fedha. Na Mpigapicha Wetu

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imehairisha kesi inayomkabili mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Ndama Shaaban Hussein, maarufu ‘Pedeshee Ndama Mtoto ya Ng’ombe’.

Ndama aliwahi kununua nyumba ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa mwaka jana kwa mnada.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Victoria Nongwa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Leonard Challo, alidai mahakamani hapo kuwa upande wa Jamhuri haujapata jalada la mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyo kutoka Jeshi la Polisi na hawawezi kuzungumza lolote.

Mbali na hilo, mwendesha mashtaka huyo alidai upelelezi bado haujakamilika na aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa kutajwa tena.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 6, mwakani itakapotajwa. Mshtakiwa alirudishwa rumande.

Ndama alifikishwa mahakamani hapo Novemba 29, mwaka huu akikabiliwa na makosa sita, likiwamo la utapeli na kutakatisha fedha Dola za Marekani 540,390 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.3.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda makosa hayo katika vipindi tofauti, ikiwamo Februari 20, 2014 mkoani Dar es Salaam.

Mbali na hilo, pia anadaiwa kutengeneza nyaraka feki, zikionyesha alipata kibali cha kusafirisha sampuli za madini ya dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles