31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DK. SHEIN AZIPONGEZA CUBA, OMAN

Na Mwandishi Wetu-ZANZIBAR


 

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman katika Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, anayefanyia kazi zake Zanzibar, Ahmed bin Humoud Al Habsi, baada ya kumtembelea Ikulu mjini Unguja jana kujitambulisha. Picha na Ikulu
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anayefanyia kazi zake Zanzibar, Ahmed bin Humoud Al Habsi, baada ya kumtembelea Ikulu mjini Unguja jana kujitambulisha. Picha na Ikulu

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amezipongeza Serikali ya Oman na Cuba kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza miradi ya maendeleo sambamba na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati alipokutana na mabalozi wa nchi hizo Ikulu mjini Unguja jana, Dk. Shein alizipongeza nchi hizo kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria ambao umekuwa chachu katika kuimarisha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kujileta maendeleo.

Akizungumza na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Jorge Tormo, walisisitiza haja ya kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo.

Balozi Tormo alimuhakikikishia Dk. Shein kuwa Cuba inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar na kuahidi kuendelea kuudumisha.

Alisema miradi yote ya maendeleo inayoishirikisha nchi yake itaendelezwa kwa juhudi kubwa, huku akimweleza Dk. Shein kuwa nchi yake itafarajika kwa kuwapo ushirikiano katika sekta ya utalii.

Mapema, Dk. Shein alifanya mazungumzo na Balozi mdogo mpya wa Oman, Ahmed bin Humoud Al Habsi, na kutumia fursa hiyo kuipongeza nchi hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo.

Kwa upande wake, Balozi Al Habsi aliyechukua nafasi ya Balozi Ali Abdulla Al Rashdi aliyemaliza muda wake wa kazi, alieleza kuwa Oman itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Zanzibar na kupongeza hatua za maendeleo zilizofikiwa hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles