27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

NGASSA DIMBANI JUMAMOSI KUIVAA MBAO

Football - Absa Premiership 2015/16 - Free State Stars v University of Pretoria - Goble Park

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa, aliyesajiliwa na klabu ya Mbeya City katika dirisha dogo, ataanza kuichezea rasmi timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC, utakaopigwa Desemba 31, mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ngassa, aliyewahi kuichezea timu ya Yanga kabla ya kujiunga na Free State Stars ya Afrika Kusini, alishindwa kuichezea timu hiyo katika michezo miwili ya mzunguko wa kwanza wa ligi kutokana na kuchelewa kufika kwa Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka klabu ya Fanja FC ya Oman.

Ngassa alijiunga na Fanja FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Oman Septemba mwaka huu, baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Free State Stars.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten, alisema ITC ya mshambuliaji huyo tayari imewasili na sasa ni jukumu la kocha Kinnah Phiri kumpanga katika michezo iliyobaki.

“Tulitegemea ITC itafika mapema tangu wiki iliyopita, lakini ikashindikana na badala yake tukaipata jana (juzi) usiku, hivyo kwa sasa yupo huru kucheza,” alisema.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbao, Ten alisema wachezaji wanaendelea kufanya mazoezi ili kujiweka fiti na kuhakikisha ushindi unapatikana, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana katika michezo miwili mfululizo.

Nyota huyo wa zamani wa klabu za Yanga, Azam FC, Simba na Kagera Sugar, alijiunga na klabu ya Fanja FC kwa muda mfupi na baadaye kuamua kurejea nchini na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mbeya City.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles