23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

MOURINHO: IBRAHIMOVIC ATAZEEKEA MAN UNITED

Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, amedai kuwa mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic, ataendelea kucheza soka ndani ya klabu hiyo hadi pale atakapotangaza kustaafu kwake.

Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na klabu za nchini China au Marekani, lakini Mourinho amedai kuwa, hizo ni habari ambazo zinatengenezwa, hivyo mchezaji huyo hawezi kuondoka.

Kocha huyo alimsajili Ibrahimovic na kujiunga na Old Trafford wakati wa majira ya joto mwaka huu, baada ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, hivyo Mourinho anaamini hawezi kuangushwa na mchezaji huyo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao 16 katika michezo 25 aliyocheza akiwa na klabu hiyo tangu ajiunge mwaka huu.

“Nina furaha na amani kuwa na mchezaji huyo ndani ya kikosi, nadhani kuna watu wanaangalia jinsi mchezaji huyo alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao akiwa nchini Ufaransa, lakini huku wanaona kama hakuna lolote.

“Kwa upande wangu ninaamini kuwa ana uwezo wa kufanya makubwa kama yale ambayo alikuwa anayafanya nchini Ufaransa.

“Hapa kwa sasa anafunga mabao na anatoa mchango mkubwa, nina furaha kwa kuwa ninaamini ataendelea kuwa hapa hadi pale atakapotangaza kustaafu soka lake. Sina imani kama mchezaji huyo atastaafu soka huku akizitumikia klabu za nchini China au Marekani.

“Mchezaji huyu amekuwa akifunga mabao mara kwa mara kutokana na uwezo wake, lakini wapo wachezaji wakubwa duniani ambao hadi wanakuwa wafungaji bora ni kutokana na mabao yao ya penalti.

“Katika michezo yote aliyocheza akiwa na klabu hii amepiga penalti moja, lakini mabao mengine yote ni kutokana na uwezo wake.

Mourinho amedai, kutokana na kufanya kazi na mchezaji huyo tangu akiwa na umri wa miaka 25, 26 na 27, sasa anafanya naye kazi tena, huku akiwa na umri wa miaka 35, basi ni lazima ataendelea kuwa naye hadi kustaafu kwake.

“Imani yangu kubwa ni kwamba, nitaendelea kuwa na mchezaji huyo hadi kustaafu kwake, kwa kuwa nilianza kufanya naye kazi tangu akiwa na umri mdogo na sasa ana umri mkubwa, hivyo hata kama akistaafu basi atakuwa chini yangu,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles