27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

KAGAME APATA MPINZANI UCHAGUZI WA RAIS 2017

17008707821_4d25809c36_k

KIGALI, RWANDA

MWANASIASA wa upinzani nchini Rwanda, Frank Habineza ameteuliwa na chama chake cha Democratic Green Party of Rwanda (DGPR) kumkabili Rais Paul Kagame katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mapema Agosti 2017.

Kwa kitendo hicho, chama hicho cha Kijani kimeachana na tishio lake la awali la kutaka kususia uchaguzi huo baada ya madai yake ya kufanyika mabadiliko ya sheria za chaguzi kupuuzwa na serikali.

Kikieleza mabadiliko ya mkakati wake, Wakijani kama kinavyojulikana kilieleza kuwa ushiriki katika uchaguzi huo una manufaa kuliko kuususia.

Chama hicho kimekuwa cha kwanza cha upinzani kumteua mgombea wa urais, na mgombea huyo anakuwa wa pili baada ya Rais Kagame.

Kagame aliashiria kushiriki uchaguzi huo tangu mapema mwaka huu baada ya mabadiliko ya katiba kumruhusu kuwania urais kwa muhula wa tatu.
“Tunataka kuleta demokrasia kwa nchi hii. Demokrasia haiwezi kuja kutoka mbinguni, haitakuja kutoka Amerika na Uingereza, ni sisi wenyewe tunaopaswa kuipigania,” Habineza alisema wakati akitoa neno la shukrani kwa kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho.

Chama hicho pia kilikuwa pekee kilichokuwa kikipinga mageuzi ya katiba, ambayo yalipitishwa rasmi Desemba 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles