28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

WANAOHAMASISHA USHOGA KUFICHULIWA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

NA WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema makanisa na misikiti vitapewa kipaumbele katika usajili kuliko baa huku akiwataka wananchi kufichua vikundi au taasisi zinazopiga kampeni ya kuhalalisha vitendo vya ushoga.

Mwigulu alizungumza hayo jana, kwenye idaba ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Kimara, jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa kuwa wizara yake ndiyo inayohusika katika jambo hilo, atahakikisha maombi yanayotumwa kwa ajili ya usajili wa nyumba za ibada yanafanyiwa kazi haraka kwa wale wanaotimiza masharti yaliyowekwa.

Alieleza kuwa anaamini uwepo wa nyumba nyingi za ibada katika maeneo mbalimbali inasaidia kuwatoa watu katika maovu na kuwaepusha vijana na makundi maovu kama kujihusisha dawa za kulevya.

“Hata mikoa yenye nyumba nyingi za ibada, ukiangalia jamii yake ni tofauti na ile iliyopo kwenye maeneo yasiyokuwa na nyumba za ibada,” alisema Mwigulu na kuongeza kuwa.

“Nilikuwa nagombana na watendaji wangu baada ya kuona kuna maombi mengi ya usajili wa nyumba za ibada hayajafanyiwa kazi, nikawaambia wanaotimiza masharti yaliyopo wapewe usajili hakuna kizuizi ni bora liwepo kanisa na msikiti kila baada ya nyumba mbili mtaani kuliko baa,” alisema.

Aidha amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kufichua taasisi zinazopiga kampeni kuhusu ndoa za jinsia moja na ushoga ili wachukuliwe hatua na ikibainika anayefanya hivyo ni mgeni atarudishwa kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles