29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

JAFFO: WALIOTAFUNA MIL 300/- WACHUKULIWE HATUA

Na FLORENCE SANAWA-MTWARA


seleman-jafoNAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, ameagiza watumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani waliohusika kutumia zaidi ya Sh milioni 300 za miradi ya ujenzi wa shule na barabara wachukuliwe hatua za kisheria.

Kauli hiyo, ameitoa jana wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Mkoa wa Mtwara na kubaini uwapo wa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alisema fedha hizo zilizokuwa zimetengwa kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Umoja, zimeliwa na wajanja.

“Hawa watu waliokula fedha za miradi, tuwapeleka mahakamani… haiwezekani fedha zote za wananchi ziliwe kisha watu wapo tu wanaishi, wanahamishwa hapa wanapelekwa sehemu nyingine, wote waliofanya hivi hawatavumiliwa.

“Haiwezekani mtu anatafuta mamilioni ya fedha kiasi hiki… hii itakuwa ni ‘network’, tutawatafuta mmoja baada ya mwingine, wa kwanza hadi mwisho, hata kama kuna viongozi wa kisiasa walishiriki  tutawachukulia hatua,” alisema Jafo.

Alisema fedha za makusanyo ya ndani zilipaswa kutumika kwa maendeleo ya wananchi na kukata asilimia tano ya vijana na wanawake ili wapatiwe mikopo.

Jafo alisema  aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, ambaye  amehamishiwa Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa, Limbakisye Shimwela na aliyekuwa mwekahazina, Christina Buchuma, lazima wachukuliwe hatua.

kwa upande wake, Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Beatrice Dominic, alisema baada ya kukuta taarifa ya matumizi ya fedha ambayo haijaainishwa, alichukua uamuzi wa kumpumzisha kazi mwekahazina huyo ili apishe uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles