32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU DK. MALASUSA AONYA

Dk. Alex Malasusa
Dk. Alex Malasusa

Na GUSTAPHU HAULE, PWANI

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, amewataka Watanzania watii mamlaka zilizopo madarakani.

Amesema kwamba, kitendo cha watu kupinga mamlaka hizo bila sababu za msingi ni sawa na kupinga uamuzi wa Mungu, kwa kuwa viongozi hao wanafanya kazi kwa kumtanguliza Mungu.

Askofu Dk. Malasusa alitoa kauli hiyo jana, wakati akifungua mkutano mkuu wa 33 wa Dayosisi ya Kanda ya Mashariki na Pwani, uliofanyika katika Shule ya Seminari iliyopo wilayani Kisarawe.

“Mwaka 2015, Tanzania ilikuwa na tukio kubwa la uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani na kufanikiwa kumpata Rais, Dk. John Magufuli.

“Kutokana na jinsi uchaguzi ulivyokuwa, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuumaliza uchaguzi huo salama.

“Kinachotakiwa sasa ni Watanzania kuheshimu mamlaka iliyoko madarakani kwa sababu imewekwa na Mungu,” alisema Askofu Dk. Malasusa.

Pamoja ya hayo, aliwataka washirika wa kanisa hilo pamoja na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwaombea viongozi walioko madarakani, ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano ili waweze kuendesha nchi kikamilifu.

“Viongozi tumewapata na wanafanya kazi vizuri. Lakini, lazima tuwatii wenye mamlaka kwa kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu wa kulipa kodi na hata ushuru, kwani kwenda kinyume ni sawa na kumpinga Mungu,” alisema Malasusa.

Aliongeza kuwa, dayosisi yake inapata mafanikio mazuri kwa ajili ya kushirikiana na Serikali na kwamba wataendelea kuiombea nchi na viongozi ili Taifa liendelee kuwa na amani.

“Lazima washirika wakatae vurugu zinazoashiria  kupoteza amani, maana kuna madhehebu yanayokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa kutoa mambo yanayokwenda kinyume na maadili,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles