23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WATU WANANE MBARONI KWA KUUZA SAMAKI WACHANGA

1

Na EMMANUEL IBRAHIM,

IDARA ya Uvuvi mkoani Geita imekamata matenga 10 ya samaki wachanga wa thamani ya Sh milioni tatu katika Halmashauri ya Mji wa Geita.

Samaki hao walikuwa  wakiingizwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa, kinyume cha sheria.

Walikamatwa juzi katika operesheni  ya kutokomeza uvuvi haramu.

Samaki hao walikuwa wanasambazwa kwenye masoko ya Nyankumbu, Shilabela na Soko la mjini Geita.

Ofisa Mfawidhi mdhibiti ubora wa samaki na msimamizi wa raslimali za uvuvi, Shafii Kitery alisema   samaki hao walikamatwa kunatokana na taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Alisema wananchi hao walieleza kuwapo  wafanyabiashara waliokuwa wakivua samaki wachanga   chini ya sentimita 50 hivyo ukawekwa  mtego na   kuwakamata.

“Ninashukuru ushirikiano wa wananchi ambao wametoa taarifa hizi.

“Hii ni hatua  endelevu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Mwanza akitaka kupambana na uvuvi haramu na kuwalinda samaki wachanga.

“Masoko yote   Geita tutayafanyia uchunguzi na kuhakikisha hawa samaki wachanga hawauzwi.

“Watu wanane tuliowakamata tunawafikisha kwenye vyombo vya sheria   vichukue mkondo wake,” alisema Kitery.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles