25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER: ARSENAL TUMEVUNA TULICHOKIPANDA

LONDON, ENGLAND


 

wenger-arseneBAADA ya klabu ya Arsenal kuchezea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Southampton juzi, kocha wa klabu hiyo amedai wamevuna walichokipanda.

Katika mchezo huo, Arsenal walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Emirates, lakini walikubali kichapo hicho kwenye mchezo huo wa Kombe la Ligi hatua ya robo fainali.

“Ni wazi kwamba tumeshindwa kuwapa mashabiki kile ambacho walikitarajia, kutokana na hali hiyo walistahili kutuzomea.

“Tumecheza chini ya kiwango hasa katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, naweza kusema kwamba safu yetu ya ulinzi haikuwa imara na ndio maana wakaruhusu mabao kirahisi.

“Kipindi cha pili tulionekana kuwa bora na kucheza mpira wa matumani lakini bado hatukuweza kufanya vizuri, naweza kusema ulikuwa usiku mbaya kwetu kwa kucheza saa mbili bila ya kupata bao.

“Tumevuna tulichokipanda, tulijisahau kipindi cha kwanza, hivyo wenzetu waliweza kutumia nafasi vizuri,” alisema Wenger.

Wenger amefungwa na kocha wa Southampton, Claude Puel ambaye alikuwa ni mchezaji wake wa zamani katika klabu ya AS Monaco, kuanzia mwaka 1987 hadi 1994.

Kwa upande wa Southampton, ni mara yao ya kwanza kufanikiwa kuingia robo fainali katika michuano hiyo ya Kombe la Ligi kwa miaka 30, hivyo Puel ameweka historia mpya.

Mchezo mwingine ni Manchester United ambao walikuwa kwenye Uwanja wa Old Trafford na kufanikiwa kushinda mabao 4-1 dhidi ya West Ham na kuingia nusu fainali, huku mabao ya Man United yakiwekwa wavuni na washambuliaji wao, Anthony Martial na Zlatan Ibrahimovic, kila mmoja akifunga mabao mawili.

Kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho ambaye hakuwepo kwenye benchi kutokana na kufungiwa mchezo mmoja, alimmwagia sifa mchezaji wake, Henrikh Mkhitaryan, kutokana na kiwango alichokionesha.

Mchezaji huyo alifanikiwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo. “Nimevutiwa na kiwango cha Mkhitaryan, anastahili sifa kwa kuwa amecheza na timu ambayo inashiriki ligi kuu na ameonesha kiwango cha hali ya juu,” alisema Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles