28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

UN YAIWEKEA VIKWAZO VIKALI KOREA KASKAZINI

NEW YORK, MAREKANI


 Samantha Power
Samantha Power

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limeiwekea vikwazo vikali Korea Kaskazini kutokana na nchi hiyo kufanya jaribio la nyuklia Septemba mwaka huu.

Hiyo ni awamu ya pili ya vikwazo dhidi ya nchi hiyo mwaka huu.

Azimio hilo ambalo lina vipengee vingi vya kiufundi, lilifikiwa baada ya miezi mitatu ya mazungumzo kati ya Marekani na China.

Linalenga mapato ya kigeni ya Korea Kaskazini na kutaka kuziba mianya katika vikwazo vilivyopo.

Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea Kusini imesema nchi yake imefurahishwa na hatua ya baraza hilo.

Hatua hizo mpya zinalenga mauzo ya nje ya makaa ya mawe kutoka Korea Kaskazini, ambayo yanaipatia nchi hiyo karibu theluthi ya mapato yake.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power, ameliita azimio hilo kuwa linaloweka vikwazo vigumu zaidi, ambavyo haijawahi kuviweka dhidi ya nchi yoyote katika kipindi kirefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles