LONDON, ENGLAND
MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajia kuendelea wiki hii hatua ya makundi, huku michezo nane ikitarajiwa kupigwa kwenye viwanja tofauti leo hii.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Leicester City, watakuwa katika uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha Club Brugge.
Katika mchezo wao wa mwisho katika michuano hii, wiki moja iliyopita Leicester City ilishuka dimbani dhidi ya Kobenhavn ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kutofungana.
Katika mchezo wa leo, kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri, amedai kuwa ni lazima timu yake iingie uwanjani kwa ajili ya kutafuata alama tatu ili waweze kuwa sehemu nzuri zaidi kwa kuwa hadi sasa wameshinda michezo mitatu, huku wakitoka sare mchezo mmoja tangu kuanza kwa hatua ya makundi.
Klabu ya Sevilla ambayo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania, leo hii itakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao Juventus.
Wawili hao walikutana katika mchezo wa kwanza kabisa katika hatua ya makundi ambapo timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, lakini hadi sasa Sevilla imeshinda jumla ya michezo mitatu na sare moja, wakati huo Juventus ikishinda michezo miwili na sare mbili.
Huu ni mchezo mgumu kwa kila upande kwa kuwa kila timu inataka kushinda ili kujiweka sawa katika msimamo wa michuano hiyo.
Monaco watakuwa nyumbani kuwakaribisha Tottenham, katika mchezo wa awali Tottenham walikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Monaco kwenye uwanja wa nyumbani, leo hii Tottenham wanatarajia kuwafuata wapinzani hao.
Monaco imeshinda michezo miwili na kutoa sare mbili tangu kuanza kwa hatua hiyo ya makundi, wakati huo Tottenham ikishinda mchezo mmoja na kufungwa michezo miwili, huku ikitoa sare mchezo mmoja, hivyo mchezo wa leo unaonekana kuwa utakuwa mgumu kwa kuwa Tottenham inahitaji ushindi.
Michezo mingine ambayo itapigwa usiku wa leo ni pamoja na CSKA Moscow dhidi ya Bayer, Kobenhavn dhidi ya Porto, Dinamo Zagreb dhidi ya Lyon, Dortmund dhidi ya Legia Warsaw, huku Real Madrid ikicheza na Sporting