25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

WAKONGWE CCM WAMSHAURI WASIRA AACHANE NA KESI

NA SHOMARI BINDA- MUSOMA


 

steven-wasira

WANASIASA wakongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamemshauri aliyekuwa Mbunge wa zamani wa   Bunda mjini,Stephen Wasira, kuachana na kusudio lake la kutaka kukata rufaa kuendelea na kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MTANZANIA juu ya kusudio hilo la Wasira, walisema itakapokatwa rufaa itachukua tena mwaka kuweza kusikilizwa   shauri mahakamani na hivyo kushindwa kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa  Bunda mjini.

Diwani mstafu wa Kata ya Mwigombero   mjini Musoma aliyeitumikia nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 25 kupitia  ,Selemani Kerenge ,alisema imefika wakati wa   Wasira, kupumzika na kuendelea kutoa ushauri   anapoona ili kuwasaidia wananchi kufikia maendeleo wanayoyataka.

Alisema Wasira ni kiongozi mkongwe ambaye yapo mambo mengi ambayo anayajua na kuweza kuyatolea ushauri ambako kupitia viongozi waliopo sasa watamtumia kuweza kuyafikia malengo.

Kerenge alisema ni vizuri mwanasia huyo akazingatia ushauri uliotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu aliyehukumu kesi namba 1 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Bunda mjini ikiwa ni pamoja na kukaa chini sasa na kwa pamoja kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa Bunda.

Alisema alianza siasa na Wasira tangu mwaka 1970 akigombea Jimbo la Mwibara na yeye akigombea Nyanja.

Kerenge alisema  Wasira alipitishwa na chama huku yeye akiondolewa kugombea kutokana na umri wake kuwa mdogo licha ya kushinda hatua za awali.
Alisema ameshika nafasi nyingi ndani ya CCM akiwa na Wasira na anamfahamu vizuri.

Diwani huyo mstaafu alisema  kila zama zina nyakati zake za uongozi na akamuomba Wasira abaki kama mzazi na mshauri na kuacha mapambano ya siasa   na vijana katika kuwania madaraka.

“Mimi ushauri wangu kwa mzee Wasira ni kumuomba  kuachana na kusudio lake la kutaka kukata rufaa juu ya uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu maana kutazidi kuchelewesha maendeleo.

“Rufaa ni haki ya mtu kuweza kukata anapoona inafaa lakini kwenye shauri hili la uchaguzi ningemuomba kiongozi mwezangu kuachana na kusudio na kushirikiana na viongozi katika kutoa ushauri katika kusukuma mbele maendeleo,” alisema Kerenge.

Alisema Wasira amepitia madaraka makubwa tangu awamu ya kwanza hadi ya nne ya uongozi wa serikali.

Kerenge alisema kila chenye mwanzo kina  mwisho   na akaziomba kamati za maendeleo kwenye vikao vyake kumualika kama mshauri kutokana na nafasi alizopitia.

“Muda wa mimi na Wasira umeisha na ni vema tukabaki washauri ndani ya chama na serikali.

“Mapambano haya yatawafanya watu hata kukichukia chama na serikali yake iliyopo madarakani,”aliongeza.

Mmoja wa viongozi wakongwe wa CCM katika   Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alisema kilichobaki ni kujipanga na uchaguzi wa mwaka 2020 ili kuwafanya wananchi wasikichukie chama kutokana na kesi hizo.

Alisema wakati uliopo ni vema kukaa chini na kuona ni wapi walipojikwaa kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na kupoteza jimbo hilo na kuanza maandalizi ya kuingia kwenye uchaguzi ujao.

Katika hukumu iliyosomwa na Jaji Noel Chocha, Novemba 18 alimthibitisha Esther Bulaya kuwa mbunge halali wa Bunda mjini.

Aliitaja Wilaya ya Bunda   kama wilaya masikini ambako viongozi wanapaswa kushirikiana   kusukuma mbele maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles