26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

OFISA MTENDAJI AKAMATWA AKIDAIWA KUBAKA MWANAFUNZI

Na PETER FABIAN – MWANZA


rape-reu-759

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikiria Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, James Chirangwile (42), kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 11 wa shule ya msingi Nyaburogoya Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Augustino Senga, alisema tukio hilo lilitokea Novemba 16, mwaka huu   katika   mtaa wa Mkuyuni.

Ilidaiwa  Mtendaji huyo   alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo (jina tunalihifadhi) na kumkuta akiwa ndani.

Kamanda alisema  baada ya mtuhumiwa kubaini kuwa mwanafunzi huyo alikuwa peke yake alimdanganya na  kuingia ndani ambako alimfanyia unyama huo na kuondoka haraka kabla ya wazazi na ndugu wa mwanafunzi huyo hawajarejea nyumbani hapo.

“Siku hiyo mtuhumiwa aliondoka na haikujulikana hadi kesho yake asubuhi mwanafunzi huyo alipofika shule ya msingi Nyaburogoya   Kata ya Mkuyuni,  mwalimu wa darasa alimuona mwanafunzi huyo akitembea kwa shida akionekana kuwa na maumivu,” alisema.

Kamanda  alisema kwa baada ya mwalimu kumbana mwanafunzi huyo alidai alibakwa na jirani yao aliyemtaja kwa jina la Chirangwile.

“Basi taarifa hiyo mwalimu aliipeleka kwa mwalimu mkuu kabla ya kuwaeleza wazazi wa mwanafunzi huyo ambao walikwenda Kituo cha Polisi Kata ya Igogo.

“Waliweza kumkamata mtendaji huyo ambaye anashikiliwa kwa mahojiano na kusubiri uchunguzi zaidi na taarifa ya daktari alipopelekwa kufanyiwa uchunguzi mwanafunzi huyo,”alisema.

Senga alisema polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo pamoja na kupitia ripoti ya daktari kabla ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Kamanda Senga aliwataka wananchi wajenge tabia na mazoea ya kuzungumza  na watoto wao wa kike   wanapowaona wakiwa na muonekano wa tofauti na siku zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles