28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

LINDI, MTWARA ZAONGOZA MIMBA ZA UTOTONI

NA FLORENCE SANAWA -MTWARA


ummy-mwalimu

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mikoa ya Lindi na Mtwara  imekuwa ikiongoza kwa watoto wadogo kushika mimba.

Alisema katika Mkoa wa Lindi katika  wasichana  100,  29 hupata ujazito mapema wakati mkoani Mtwara, wasichana 100 kati yao 30 hupata ujauzito kabla ya umri wa miaka 18.

Waziri alisema hali hiyo husababisha ongezeko la vifo vinavyotokana  na uzazi.

Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Tumaini la Mama unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) na kusimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani hapa.

Waziri aliwataka wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kutoa elimu kwa watoto wao itakayokupunguza mimba za utotoni.

Hatua hiyo itachangia kupungunza vifo wakati wa kujifungua na kuwaondoa katika hatari zaidi, alisema.

Akizungumzia mradi huo, alisema utafanya kazi kwa  miaka miwili na utasaidia wajawazito na watoto kabla ya kujifungua na baada, ikiwa ni sehemu ya kumkinga mama na mtoto.

“Mradi huu si tu utaboresha huduma za mama na mtoto pekee bali hata   watumishi wanapaswa wabadilike.

“Wale watakaokuwa na lugha chafu mtuambie tuwashughulikie, hatutaweza kuhangaikia maboresho ya afya halafu mhudumu mmoja akatuangusha, hilo sitakubali.

“Mradi huu usiwe chachu ya kuhimiza wanawake kuzaa mara kwa mara na kushindwa kuepuka vishawishi hali ambayo itasababisha watoto kukosa lishe ya kutosha ama kuongeza mimba kwa watoto.

“Hatutakuwa tumetenda haki kwa mradi huu,” alisema Ummy.

Alisema wazazi lazima wajikite kutoa elimu kwa watoto wao.

Takwimu za mwaka 2005 zinaonyesha  Lindi na Mtwara ipo katika mikoa 10 inayoongoza kwa mimba za utotoni.

“Hizi taarifa zitukumbushe wajibu wetu ili kupunguza kiwango hicho kitakachosaidia kuwaondoa watoto katika hatari wakati wa kujifungua,” alisema Mwalimu.

Mwakilishi wa Balozi wa Ujerumani nchini, Julia Hanning, alisema serikali ya Ujerumani hutumia wastani wa Sh bilioni 17 hadi Sh bilioni 41 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Tanzania.

Alisema hadi sasa asilimia 60 ya wanawake wanajifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 43 iliyokuwapo miaka iliyopita huku vituo vitakavyofikiwa na mradi vitapata nafasi ya kuongeza mapato katika kipindi chote cha mradi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles