27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

KAMANDA SIRRO AKAMATA WAUZA SHISHA WATATU

Na HERIETH FAUSTINE – DAR ES SALAAM


dscf2219

JESHI la Polisi Kanda ya Kinondoni linawashikilia wafanyabiashara watatu kwa uuzaji wa shisha ambao ulipigwa marufuku na Serikali kwa vile una madhara kwa watumiaji.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  kumtuhumu  Kamanda  wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Suzzana Kaganda.

Makonda alidai   huenda viongozi hao walipokea rushwa ya Sh milioni 50 kutoka  kwa kikundi cha wafanyabiashara 10, hali iliyosababisha kushindwa kuwakamata wauzaji wa kilevi hicho.

Makonda alitoa  tuhuma hizo akisema  rushwa hiyo ndiyo inawafanya Sirro na Kaganda walegelege kuwakamata wafanyabiashara hao waliomfuata ofisini kwake, licha ya kuwaagiza kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Kamanda Sirro alisema wafanyabishara hao walikamatwa wakiwa na vielelezo ambavyo vinatarajiwa kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi.

“Watu watatu ambao ni wafanyabiashara  wa shisha wamekamatwa wakiwa na vielelezo na taarifa zaidi anazo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni,”alisema   Sirro.

MTANZANIA, lilimtafuta Kamanda Kaganda ambaye alikiri kukamtwa   wafanyabiashara hao wa shisha  usiku wa kuamkia jana katika maeneo ya Mikocheni.

Alisema kupitia operesheni wanayoendelea kuifanya ya kuwasaka wafanyabiashara wa kilevi cha shisha, waliwezaa kuwakamata watatu wakiwa na mashine za shisha

Alisema kutokana na upelelezi unaoendelea kufanywa kuhusiana na biashara hiyo, kwa sasa hawataweza kuyataja  majina yao kwa kuhofia kupoteza ushahidi.

Kamada alisema wafanyabiashara hao kwa sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles