32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi 3,800 hawapati majisafi

Mbuge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza
Mbuge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza

Na ELIUD NGONDO, MBEYA

WAKAZI 3,800 wa Kijiji cha Swaya  Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, hawapati huduma ya majisafi licha ya chanzo cha maji yanayotumika katika Jiji la Mbeya kuwa eneo lao.

Wananchi hao, wameiomba Serikali kuwasogezea huduma hiyo ili waondokane na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.

Wananchi hao, walitoa kilio chao hicho kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa  na Mbuge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza alipofanya ziara ya kujua kero za wapiga kura wake.

Walidai wanatumia maji ya  kutoka kwenye mito na vijito vilivyopo maeneo hayo maji ambayo walidai usalama wake ni mdogo kiafya.

Akisoma taarifa ya kijiji hicho,Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Frank Mwaibingila alisema wananchi wamekuwa wakichota maji katika mito ambayo ni hatari kwa afya zao kwa madai kuwa wanaweza kupatwa na magonwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.

Alisema kuna vyanzo vya maji katika kijiji hicho ambavyo wanaonufaika ni wakazi wa Jiji la Mbeya.

“Wananchi wetu wanaendelea kupata shida ya maji,wanalazimika kutumia maji machafu  wakati kuna vyanzo vya maji kijijini vinawanufaisha watu wa Jiji la Mbeya,wana hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko,” alisema  Mwaibingila.

Kwa upande wake,Njeza alisema wananchi kukosa huduma ya maji wakati wao ndiyo wanaotunza chanzo cha maji yanayotumika sehemu nyingine ni kutowatendea haki.

Alisema pamoja na hilo,Serikali inatakiwa kuhakikisha inawasaidia kuwapatia huduma ya maji na sio kutunza chanzo hicho.

“Haiwezekani wananchi wangu waendelee kupata shida,wakati wao ndio wanao tunza vyanzo vya maji ambayo watu wa Jiji la Mbeya wanatumia,Serikali ilishughurikie suala hili haraka,” alisema Njeza.

Alimtaka  Kaimu Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mwachembe Shizya kutoa maelezo ya kitaalamu sababu zinazokwamisha wananchi hao kukosa huduma.

Shizya alisema Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji hicho na kwamba kilichokwamisha ni mkandarasi wa awali kukimbia na fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles