22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani wagomea mpango wa JPM

Rais Dk. John Magufuli
Rais Dk. John Magufuli

Na AMINA OMARI, MUHEZA

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga, wamegoma kupitisha mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mashamba matano ya mkonge yaliyofutwa na Rais Dk. John Magufuli mwanzoni mwa mwaka huu.

Madiwani hao wamechukua uamuzi huo baada ya kuhisi kuwapo kwa harufu ya rushwa katika mpango huo pamoja na kutoshirikisha wataalamu ngazi ya wilaya katika uandaaji wa taarifa za tathmini ya wananchi wanaozunguka mashamba husika.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bakari Mhando, alisema madiwani hawakuridhishwa na mpango huo kwani umeandaliwa bila kuwashirikisha wenye mamlaka ambao ni madiwani.

Kwa mujibu wa Mhando, Baraza la Madiwani ndilo lenye haki ya kupitisha matumizi ya ardhi katika eneo husika na kwamba utaratibu unapofanyika kinyume na hapo, unakuwa unakiuka sheria.

“Kama tutaupitisha mpango huu, utaweza kutuletea migogoro ya ardhi isiyokwisha katika halmashauri yetu kwani takwimu zilizotumika za wananchi wanaoishi karibu na mashamba hayo si sahihi.

“Kwa mfano, shamba la Lewa lina wakulima ambao tayari wanalima zaidi ya ekari 20 katika mpango uliopo, mkulima anatakiwa apewe ekari moja, jambo ambalo litaweza kutuletea madhara kwa siku zijazo,” alisema Mhando.

Naye Diwani wa Kata ya Nkumba, Charles Mhilu, alisema kuna majina yameshaorodheshwa katika shamba la Kibaranga wakati halmashauri hiyo haina taarifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles