25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kupeleka umeme jimboni kwa Bashe

husein-basheSERIKALI imesema inaendelea kutekeleza miradi ya umeme katika maeneo yote ya vijijini ikiwa ni pamoja vijiji vya Jimbo la Nzega Mjini.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medad Kalemani alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nzega Mjini, Husein Bashe (CCM), aliyetaka kujua vijiji vya Mwanzole, Bulunde na Kashishi vilivyopo jimboni kwake vitapelekewa umeme lini na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) awamu ya tatu.

“Kwa kuwa matatizo ya Jimbo la Nzega Mjini yanafanana na yale ya Mufindi Kusini, namwomba waziri anipatie majibu ni lini vijiji vya Mwanzole, Bulunde na Kashishi vitapata umeme,’’ alihoji Bashe.

Akijibu swali hilo, Dk. Kalemani alisema Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kufikisha umeme katika maeneo yote ya vijijini ikiwamo katika Jimbo la Nzega linaloongozwa na Bashe.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola (CCM).

Katika swali lake, Kigola alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka umeme katika kata za Idete, Idunda, Kiyowelo, Maduma na Mtambula ili wananchi waweze kufaidika na huduma hiyo.

Akijibu swali hilo, Dk. Kalemani alisema Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kufikisha umeme katika maeneo yote nchini ikiwa ni pamoja na vijiji vya Mufindi Kusini.

Alisema kwamba, vijiji vya Kata ya Idete, Idunda, Kiyowela, Maduma na Mtambula, vitapatiwa umeme kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu.

Alisema kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji hivyo pamoja na katika Wilaya ya Mufindi, itahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 81 na ufungaji wa trasfoma 24 pamoja na kuwaunganishia umeme wateja 3,533 wa awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles