32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hukumu kesi ya ole Nagole kutolewa leo

olenangoleNa JANETH MUSHI-ARUSHA

MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania inayoendelea na kikao chake jijini Arusha, leo inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa ikiyofunguliwa na Mbunge wa Longido, Onesmo ole Nangole  (Chadema), aliyevuliwa ubunge na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na jopo la majaji watatu waliosikiliza rufaa ya mbunge huyo wiki iliyopita, wakiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Sauda Mjasiri. Majaji wengine ni Mussa Kipenka na Profesa Juma Ibrahim.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Wakili wa ole Nangole, Method Kimomogoro, alisema wamepokea wito wa mahakama hiyo  ukiwajulisha uamuzi wa rufaa hiyo, kwamba utasomwa leo saa tano asubuhi.

Juni 29, mwaka huu, Mahakama Kuu ilimvua ole Nangole ubunge katika kesi ya uchaguzi namba 36 ya mwaka 2015, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Dk. Steven Kiruswa, akipinga matokeo yaliyompa ushindi ole Nangole kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Katika rufaa hiyo namba 129 ya mwaka 2016, ole Nangole anapinga uamuzi uliotolewa na Jaji Sivangilwa Mwangesi aliyetengua ubunge wake katika Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.

Ole Nangole anawakilishwa na Wakili Kimomogoro akisaidiana na Wakili John Materu wakati Dk. Kiruswa anawakilishwa na Wakili Dk. Masumbuko Lamwai, Wakili David Haraka na Wakili Edmund Ngemela.

Katika rufaa hiyo, ole Nangole anaiomba  mahakama hiyo itengue hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na imtangaze yeye kuwa ndiye mshindi halali wa kiti cha ubunge.

Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, ilianza kusikiliza kesi hiyo Februari 29, mwaka huu, ambapo Dk. Kiruswa alikuwa na mashahidi 28 na vielelezo vinane huku upande wa wadaiwa wakiwa na mashahidi tisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles