23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Basi laua 10, watalii wanusurika

ajaliAli Badi Kilwa

WATU 10 wamefariki dunia na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Barcelona kupasuka gurudumu la mbele na kupinduka katika Kijiji cha Miteja wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Tukio hilo limetokea jana saa nne asubuhi, wakati basi hilo linalofanya safari zake kati ya Tandahimba na Mtwara likitokea Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya Kilwa, Christopher Ngubiagai alilitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakagua mara kwa mara magari hayo ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Alisema umefika wakati kwa jeshi hilo, kuyazuia mabasi yasiyokuwa na sifa ya kusafirisha abiria ili kuepuka ajali.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kinyonga, Dk. Jafari Thobias alisema wamepokea mili ya watu 10 na majerui 44.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga alithibitisha  kutokea kwa ajali hiyo.

 

ARUSHA

Habari kutoka mkoani Arusha, zinasema watalii wanne na rubani wao, wamenusurika kifo baada ya ndege ya Kampuni ya Coastal Aviation aina ya Caravan 5H ZEB kuzimika injini ikiwa angani na kulazimika kutua kwenye mashamba.

Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana uwanja mdogo wa ndege wa Arusha uliopo eneo la  Kisongo nje kidogo ya mji huo, wakati ndege hiyo iliporuka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Akizungumza na Gazeti la MTANZANIA jana, Kaimu Meneja wa Uwanja huo, Bashir Labai alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema hakuna abiria aliyeumia.

Alisema ndege hiyo, iliyokuwa tayari imeruka angani dakika tano ilizima gafla injini yake ambapo rubani wake alijaribu kuigeuza na kuirejesha uwanjani.

Hata hivyo bila mafanikio akiwa anajaribu kuzunguka ndege hiyo ililazimika kushuka kwenye tambarare ya mashamba yaliyopo  pembezoni mwa uwanja huo.

“Kulikuwa na abiria wanne na rubani mmoja hawa safari yao ilikuwa ni ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro,” alisema Labai na kuongeza.

“Tunashukuru Mungu hakuna majeruhi wala aliyeumia kwani baada ya tukio hilo Kampuni ya Coastal Aviation iliyokuwa imebeba wageni hao iliwapatia ndege nyingine wakaendelea na safari yao,” alisema.

Alisema kuondoka kwa abiria hao kuelekea KIA kulitanguliwa kwanza na madaktari kuwafanyia vipimo abiria hao ili kubaini kama hawakujeruhiwa sehemu za miili yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji  wa  Kampuni  ya Coastal AIR, Kapteni Edmond Julian alishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) uwanjani hapo kwa kuwa makini.

Kuhusu abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo, Kapteni Julian aliwataja kuwa ni abiria wanne.

“Abiria  walikuwa wanne,wawili wakiwa ni raia  wa  Ujerumani na Italia walikuwa wanaekelea Zanzibar,” alisema Kapteni Julian.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles