28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Gerard Pique atangaza kustaafu soka

gerard-piqueMADRID, HISPANIA

BEKI wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Gerard Pique, ameweka wazi kuwa anatarajia kustaafu kuitumikia timu hiyo ya taifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia 2018, nchini Urusi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ameyasema hayo baada ya timu hiyo ya taifa kushinda juzi mabao 2-0 dhidi ya Albania katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

Mchezaji huyo amekuwa na furaha kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa na timu hiyo chini ya kocha Vicente del Bosque, ambapo aliweza kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2010 pamoja na michuano ya Euro 2012.

“Ninaamini Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi itakuwa ni mara yangu ya mwisho kuonekana nikiitumikia timu ya taifa.

“Nimekuwa nikifikiria jambo hilo mara kwa mara, haya si maamuzi ambayo nimeyapanga hivi sasa, ni jambo ambalo nililipanga tangu muda mrefu.

“Ninaamini wapo watu ambao wanaona ni bora nikawa nje ya timu hii kwa sasa, lakini kila kitu kina wakati wake, hivyo baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia nitafanya hivyo,” alisema Pique.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United, ameitumikia timu ya taifa kwa kucheza jumla ya michezo 85, huku akifanikiwa kupachika mabao matano.

Mara ya kwanza mchezaji huyo alichaguliwa na kikosi hicho cha Hispania mwaka 2009 Februari, kutokana na uwezo wake ambao aliuonesha akiwa na kikosi chake cha Barcelona.

Mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya England, ambapo timu yake iliweza kushinda mabao 2-0. Kutokana na hali hiyo, aliaminiwa na kupewa nafasi ya kucheza beki wa kati akiwa sambamba na Carlos Puyol.

Inadaiwa kwamba kwa sasa mchezaji huyo kiwango chake kimeanza kushuka ndani ya klabu ya Barcelona na ndio maana baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimtaka astaafu kuitumikia timu ya taifa na nguvu zake azipeleke katika klabu yake.

Mchezaji huyo hana umri mkubwa wa kumfanya astaafu soka, lakini uwezo wake umekuwa ukishuka siku hadi siku na hawezi kwenda sawa na kasi ya sasa katika soka la nchini Hispania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles