31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Ancelotti: Guardiola ameniachia kazi nyepesi Bayern

carlo-ancelottiMUNICH, UJERUMANI

KOCHA wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti, amedai kuwa ameachiwa kazi nyepesi na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola ambaye amejiunga na klabu ya Manchester City.

Ancelotti amesema kuwa anaamini atafanikiwa katika klabu hiyo ya Bayern Munich kutokana na Guardiola kuweka njia ya mafanikio ya klabu hiyo.

Guardiola akiwa katika klabu hiyo ya Bayern, alifanikiwa kutwaa mataji saba katika misimu mitatu ambayo aliitumikia ikiwa pamoja na kutwaa taji la Bundesliga.

Ancelotti amedai kuwa anavutiwa na uwezo wa wachezaji hao ambao umeachwa na kocha Guardiola.

“Ni kazi nyepesi sana kwa sasa katika klabu hii kwa kuwa nimewakuta wachezaji wakiwa katika ubora wa hali ya juu.

“Ninaamini ubora wa timu hii umeachwa na Guardiola, nimeikuta timu hii ikiwa katika ubora wa hali ya juu, hivyo sina kazi kubwa ya kuifundisha timu hii.

“Misingi ambayo imeachwa na Guardiola ninaamini siwezi kuiacha au kuibadilisha kwa sasa kwa kuwa ni mizuri na itanipa mafanikio japokuwa nina mipango yangu ambayo ninaweza kuiweka hapa,” alisema Ancelotti.

Bayern kwa sasa inashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16 huku nafasi ya pili ikishikwa na Hertha Berlin ambayo na pointi 13 baada ya timu hizo kucheza michezo sita.

“Ninajua kwamba timu yangu inafanya vizuri, nimekuwa nikiiangalia timu hii kwa misimu mitatu iliopita, hivyo kikubwa ni kuendelea na kasi hii kwa ajili ya kuipa mataji,” aliongeza.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57, aliwahi kuzifundisha klabu kubwa duniani kama vile AC Milan, Paris Saint-Germain, Real Madrid pamoja na klabu ya Chelsea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles