Na Renatha Kipaka,
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu). Salim Kijuu amesema  Serikali haitawajengea nyumba wananchi kwa sasa bali kipaumbele  ni kujenga shule na hospitali.
Alitoa ufafanuzi huo  kwa waandishi wa habari kutokana na   na malalamiko mengi ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi kutaka kujengewa nyumba.
RC alisema  kipaumbele  cha serikali ni taasisi kwa vile  wanafunzi wanatakiwa kusoma na pia hospitali zilizoharibika zinatakiwa kujengwa  ziendelee kutoa huduma katika jamii.
“Niwatake wananchi kuendelea   kuboresha miundombinu ya makazi yao ili kurudi katika hali ya zamani.
“Hatua hii ya utathmini imesiamishwa mpaka tathimini ya  awamu ya pili itakapofanyika  maana kuna wapangaji  wamekuwa wakiwaandikisha watoto wao kitu ambacho kimekwamisha hatua nzima,”alisema.
Hata hivyo alisema   wapangaji waliokuwa katika mpango wa kulipiwa kodi ya Sh 120,000 na umesimamishwa  kutokana na kutoa taarifa za uongo.
Alisema  katika  majeruhi 440  wa tetemeko lilitokea Septemba 10, mwaka huu, tayari  434 tayari wametibiwa na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao ambapo waliobaki katika hospitali mbalimbali ni sita.