
Na Renatha Kipaka,
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu). Salim Kijuu amesema Serikali haitawajengea nyumba wananchi kwa sasa bali kipaumbele ni kujenga shule na hospitali.
Alitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari kutokana na na malalamiko mengi ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi kutaka kujengewa nyumba.
RC alisema kipaumbele cha serikali ni taasisi kwa vile wanafunzi wanatakiwa kusoma na pia hospitali zilizoharibika zinatakiwa kujengwa ziendelee kutoa huduma katika jamii.
“Niwatake wananchi kuendelea kuboresha miundombinu ya makazi yao ili kurudi katika hali ya zamani.
“Hatua hii ya utathmini imesiamishwa mpaka tathimini ya awamu ya pili itakapofanyika maana kuna wapangaji wamekuwa wakiwaandikisha watoto wao kitu ambacho kimekwamisha hatua nzima,”alisema.
Hata hivyo alisema wapangaji waliokuwa katika mpango wa kulipiwa kodi ya Sh 120,000 na umesimamishwa kutokana na kutoa taarifa za uongo.
Alisema katika majeruhi 440 wa tetemeko lilitokea Septemba 10, mwaka huu, tayari 434 tayari wametibiwa na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao ambapo waliobaki katika hospitali mbalimbali ni sita.