NA KOKU DAVID-DAR ES SALAAM
WAKATI zimebaki siku tisa kumalizika uhakiki na uboreshaji wa namba za Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kwa mikoa ya kodi ya Dar es Salaam na Zanzibar, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haitaongeza muda tena.
Mamlaka hiyo imesema badala yake TIN za zamani hazitafanya kazi baada ya muda huo.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema hadi sasa TIN zilizohakikiwa ni 15,467.
Alisema kila mtu mwenye TIN anatakiwa kufika ofisi za TRA kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki kuepuka kuondolewa katika mfumo wa mamlaka hiyo.
Katika hatua nyingine, TRA imekusanya Sh trilioni 1.37 Septemba mwaka huu, huku lengo lililokusudiwa likiwa ni Sh trilioni 1.4.