29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Walioteka mabasi sita wakamatwa

bomuNa Mary Mwita, Arusha
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limewatia mbaroni watu kadhaa kwa kuhusishwa na tukio la ujambazi wa kuteka mabasi sita ya abiria yaliyokuwa yanatoka nchini Kenya kuelekea jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema katika msako huo ulioanza jana wamefanikiwa kukamata watu hao katika maeneo tofauti mkoani humo.
Kamanda Sabas alisema kwa sasa jeshi hilo haliwezi kutaja majina ya watuhumiwa hao kutokana na utaratibu wa uchunguzi unaofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi.
“Kutokana na taratibu za uchunguzi kwa sasa hatuwezi kutaja majina ya watuhumiwa tuliowakamata kwa kuhusika na tukio la ujambazi. Hadi sasa bado hatujamaliza uchunguzi wetu na pindi tukikamilisha tutawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria,” alisema Kamanda Sabas.
Alisema magari mawili kati ya sita yaliyotekwa yalikuwa na mizigo na wafanyakazi.
“Tukimaliza uchunguzi tutawapatia taarifa rasmi na kila kitu kuhusu tukio hili, ila kwa sasa tumeongeza nguvu ya ulinzi katika njia hiyo,” alibainisha Kamanda Sabas.
Alisema mabasi hayo yaliyotekwa yanamilikiwa na kampuni za Perfect, Dolphine, Taqwa na Spider ambayo yote yanafanya safari zake kati ya Arusha na Nairobi.
Kamanda Sabas alisema katika kukabiliana na uhalifu kama huo, Jeshi la Polisi litaongeza magari ya doria katika barabara hiyo inayounganisha Kenya na Tanzania.
“Kazi ya ulinzi ina changamoto nyingi kwani wahalifu nao wanabadili mbinu, eneo walikofanya utekaji ni eneo la wazi kabisa ambalo huwezi kuamini wangeweza kuteka magari, lakini tutahakikisha kuwa barabara hii inakuwa salama muda wote,” alisema Sabas.
Katika tukio hilo, dereva wa basi la Perfect alijeruhiwa jicho la kushoto baada ya kupigwa jiwe alipotaka kutoroka.
Tukio la kutekwa mabasi hayo lilitokea juzi usiku baada ya watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kuvamia na kuteka mabasi hayo katika eneo la Mbuga Nyeupe, Wilaya ya Longido.1

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles