29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

ACT wazichapa kavukavu Dar

IMG-20150119-WA0004Na Elizabeth Hombo, Dar es Salaam
VURUGU zimetokea jana kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya makundi yanayopingana ndani ya Chama cha ACT-Tanzania kukutana ana kwa ana katika ofisi hiyo kwa ajili ya kikao cha usuluhishi.
Baada ya kukutana kwa makundi hayo, ghafla walitokea vijana wanaodaiwa kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbu na kumvamia Katibu Mkuu wa muda wa chama hicho, Samson Mwigamba.
Vurugu hizo zimetokea ikiwa ni siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kumsimamisha uongozi Limbu na kumwondoa katika nafasi yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa makosa ya kinidhamu.
Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Mwigamba alidai vijana hao wamekodiwa na Limbu kwa lengo la kumfanyia vurugu baada ya kuona mikakati yake imekwama ndani ya chama.
“Limbu alikuja na kundi la vijana kama 12, kati yao wawili aliwasafirisha kwa ndege kutoka Arusha na mmoja anaitwa Gerald Emmanuel, pia alikuwamo Mwenyekiti wa Geita, Katibu Uenezi Ukonga, Katibu Uenezi Jimbo la Kinondoni pamoja na kina Mahona.
“Sasa wakati bado hatujaingia ofisini kwa msajili tukaambiwa tunatakiwa mimi na Limbu tu ndio tuingie na wengine waondoke, lakini kikundi cha Limbu hakikuondoka wakabaki pale nje wanajadiliana,” alisema Mwigamba.
Alisema wakati wamemaliza kikao na msajili, alifuatwa na Gerald huku akimshika shati lake na kumwambia anamdai fedha zake Sh milioni moja, hivyo lazima amlipe.
“Wakati tunatoka kikaoni nikawa pale nje nasubiri gari linichukue, akaja Gerald huku akishika shati langu akidai ananidai shilingi milioni moja na lazima nimlipe pale pale, nilishangaa sana na hapo ndiyo nikajua kuna kitu Limbu amefanya ili wale vijana wanivuruge na baadaye nikasirike na kuonekana nimepigana,” alisema Mwigamba.
Limbu alipotafutwa jana, alisema hakuona vurugu hizo kwani wakati huo alikuwa anazungumza na simu pembeni, na kwamba Gerald na Mwigamba wanajuana kwa kuwa wote wanatoka Arusha.
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, alisema hakushuhudia fujo hizo na kusema kwamba kuna watu wanataka kuvuruga mazungumzo yake na ACT.
“Kuna watu wanataka kuyavuruga haya mazungumzo, ndio haohao ambao wanasambaza hata picha huko kwenye mitandao ya kijamii na kukuza mambo,” alisema Jaji Mutungi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles