24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama: Wateja NSSF wasiondolewe

National_Social_Security_Fund_Tanzania_Logo

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi, imelizuia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni ya Udalali ya Majembe kuwaondoa ndani ya nyumba wakazi 87 walionunua nyumba za shirika hilo Mtoni Kijichi, Dar es Salaam hadi kesi itakapomalizika.

Amri hiyo ilitolewa jana mbele ya Jaji Penterine Kente wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakati maombi ya wakazi hao yalipotakiwa kusikilizwa.

Jaji Kente alipotakiwa kuanza kusikiliza maombi hayo, walalamikiwa ambao ni Majembe na NSSF hawakuwapo mahakamani japo walikuwa na taarifa.

Wakili wa wadai, Benito Mandele, aliomba mahakama kuahirisha maombi hayo hadi siku nyingine na itoe amri ya kuwazuia wadaiwa kuwaondoa ndani ya nyumba wateja wake.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, mahakama iliamuru NSSF na Majembe zisiwatoe ndani ya nyumba wakazi 87 hadi maombi yao yatakaposikilizwa.

Jaji Kente aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza maombi hayo.

Wakazi hao walionunua nyumba 87 zikiwa mbovu ambazo zipo maeneo yasiyokuwa na huduma za jamii, wanaiomba mahakama kuiamuru Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF kurejea mikataba, kutambua majukumu ya msingi ya kila upande na nyumba ziwe za kuwawezesha kuishi na kuwe na huduma za kijamii.

Wadaiwa katika kesi hiyo, ni Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF na Kampuni ya Majembe Auction Mart.

Wadai kupitia wakili wao, waliamua kukimbilia mahakamani kufungua kesi baada ya kushindwa kupata ufumbuzi wa madai yao katika Taasisi ya Usuluhishi kutokana na walalamikiwa kutofika.

Wanadai walifikisha suala hilo katika usuluhishi kutokana na mkataba wao kuwataka kufanya hivyo kabla ya kuamua kwenda mahakamani.

Katika madai waliyowasilisha mahakamani, wanadai mdaiwa wa kwanza ambaye ni Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, ameshindwa kutekeleza matakwa ya mkataba kwa mradi huo kukosa huduma za kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles