23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

NHC yataja vinara wakwepa kodi ya pango majengo yake

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi mkoani Dodoma, baada ya Serikali kutangaza kuhamia mkoani humo. Kulia ni Meneja katika ofi si ya mkurugenzi mkuu, Muungano Saguya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi
mkoani Dodoma, baada ya Serikali kutangaza kuhamia mkoani humo. Kulia ni Meneja katika ofi si ya
mkurugenzi mkuu, Muungano Saguya.

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WAKATI Serikali ikijiandaa kuhamia Dodoma, imeelezwa kuwa yenyewe ndiyo kinara wa kukwepa kulipa kodi ya pango kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Jumla ya taasisi zake 29 zimetajwa katika ukwepaji kodi huo, na tayari shirika hilo limezitaka zilipe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo.

Miongoni mwa taasisi hizo, ni Ofisi ya Rais ambayo inadaiwa zaidi ya Sh milioni 10.

Katika madeni hayo ambayo yamefikia zaidi ya Sh bilioni 9, Wizara ya Uchukuzi inatajwa kuongoza orodha ikidaiwa zaidi ya Sh bilioni 2.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi  nayo ina deni kubwa la zaidi ya Sh bilioni 2, ikifuatiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inayodaiwa zaidi ya Sh bilioni moja.

Katika orodha hiyo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inadaiwa zaidi ya Sh bilioni moja, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, inadaiwa Sh milioni 613, wakati Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inadaiwa Sh milioni 360.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema pamoja na deni hilo, zipo pia taasisi binafsi ikiwamo ile ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Alisema Mbowe ambaye anaendesha Mbowe Hotel Ltd, maarufu Club Bilicanas iliyoko maeneo ya Posta, Dar es Salaam, anadaiwa zaidi ya Sh bilioni 1.1.

“Tunaunga mkono uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma, ni mpango ambao umekuja kwa wakati mwafaka, Dodoma inakwenda kuwa mji wa kiserikali na Dar es Salaam unabakia kuwa mji wa kibiashara.

“NHC tunaenda kujenga Dodoma… tunataka kukusanya zaidi ya Sh bilioni 60 kutoka vyanzo mbalimbali ambazo zitatumika katika ujenzi wa nyumba za makazi.”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles