Na JANETH MUSHI, ARUSHA
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ameendelea kuvutana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo, baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wake.
Lema ameiomba ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha (RAS) kumsimamia na kumuonya mkuu huyo wa wilaya kwa kile alichosema anaingilia shughuli za halmashauri ya Jiji la Arusha.
Alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipozungumza na waandishi wa habari.
Msimamo huo wa Lema ni mwendelezo wa kutoelewana na mkuu huyo wa wilaya kwa kuwa hivi karibuni walichongeana mbele ya Naibu Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo, alipofanya ziara mkoani hapa.
Katika maelezo yake jana kwa waandishi wa habari, Lema alisema Gambo anaingilia majukumu ya halmashauri na kwamba tabia hiyo inarudisha nyuma utendaji wa madiwani wa halmashauri hiyo.
“DC amekuja na kiherehere sana, yaani anaingilia shughuli za halmashauri wakati akijua chama chake hapa kina diwani mmoja.