29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea akamatwa

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema)
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema)

Asifiwe George na Elias Saimon(TUDARCO), Dar es Salaam

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amehojiwa na polisi kwa   saa tatu akituhumiwa kuandika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai 25 hadi 30, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,  v Hezron Gyimbi, alisema  mbunge huyo alihojiwa  kutokana na kauli b anazozitoa katika magazeti yake.

Alisema maneno hayo ya Kubenea yanaweza kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani.

“Kutokana na kauli zake anazozitoa mara kwa mara zenye viashiria vya uchochezi ndiyo maana tumemhoji na tumemuachia kwa dhamana lakini kesho asubuhi (leo) atatakiwa kuripoti tena   kuendelea na mahojiano,” alisema Gyimbi.

Mbunge huyo wa Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi ambao ni wachapishaji wa gazeti la Mwanahalisi, Mseto lililofungiwa kwa miezi 36  na Mawio ambalo limefungwa kwa muda usiojulikana, aliwasili kituoni hapo jana saa 7.00  mchana akiwa na gari  namba   T 216 BHH Land Cruiser   akiwa ameongozana na wanasheria wake, Tundu  Lissu na Fredrick Kihwelo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lissu  alisema  mteja wake alihojiwa na polisi kuhusu makala aliyoiandika katika gazeti lake wiki tatu zilizopita ikielezea hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu Visiwani Zanzibar.

“Kwa mujibu wa polisi makala hiyo ni  ya  uchochezi na polisi walikuwa wakiuliza maswali yao ya ajabu ajabu na aliulizwa kwamba alijaribu kuonana na polisi kuhusiana na hiyo makala yake.

“Kwa kiasi kikubwa alihojiwa maswali  ambayo  majibu yake  yote yapo kwenye hiyo makala yenyewe,” alisema Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles