25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Makonda atumbua wawili mipango miji

makondaNA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewarudisha kwa Kamishina wa Ardhi, maofisa wawili wa Idara ya Mipango Miji wa Manispaa za Ilala na Kinondoni kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Maofisa waliosimamishwa kazi ni Juliana Lutara wa Manispaa ya Kindoni na Paul Mbembela wa Manispaa ya Ilala.

Makonda alisema hajaridhishwa na utendaji kazi wao hivyo  wakapangiwe majukumu mengine nje ya Dar es Salaam.

Makonda alichukua uamuzi huo jana wakati wa kikao cha madiwani wote wa   Dar es Salaam kilichoitishwa   kuainisha maeneo yote ya wazi ambayo yamevamiwa.

Aliwataka   wote ambao wamevamia maeneo ya wazi kuondoka mara moja kuanzia jana kabla hatua ya kuwaondoa haijaanza.

Alisema jukumu la kutambua maeneo yote ya wazi, shule, makanisa, makaburi ambayo yamevamiwa, linapaswa kuwa chini ya Ofisa Mipango Miji ambaye anatakiwa kufahamu takwimu sahihi za maeneo yaliyochukuliwa na si kusema kuwa suala hilo liko kwenye mchakato.

“Hili ni jambo lisilowezekana kwa maofisa mipango miji kushindwa kubaini maeneo yao.

“Hivyo huu ni uzembe wa hali ya juu na watu wa aina hii siko tayari kuwavumilia, kuanzia leo(jana) Kamishna wa Ardhi atawapangia kazi nyingine ya kufanya.

“Haiwezekani mtu ushindwe kuwa na majibu ya maeneo yaliyovamiwa wakati ndiyo idara yako huu ni uzembe wa hali ya juu,” alisema Makonda.

Alisema ni jukumu la kila kiongozi kuhakikisha anatimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwa msimamizi mkuu katika idara yake na si vinginevyo, ili kuendana na kasi ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles