24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi UDOM auawa

Kamanda-wa-Polisi-Mkoa-wa-Dodoma-Lazaro-Mambosasa1Na RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, tukio hilo lilitokea jana usiku chuoni hapo.

“Mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele za kuomba msaada na walinzi walipokwenda eneo la tukio, walimkuta akigalagala chini.

“Walinzi walimpa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini  lakini alifia njiani.

“Inavyoonekana, alipigwa na watu wasiofahamika kwa sababu  katika mwili wake  amekutwa na majeraha makubwa,’’alisema Kamanda Mambosasa.

Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho ambaye anasomea   sayansi ya jamii ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema   Fredrick alikuwa akitoka katika matembezi yake ya kawaida.

“Ulikuwa ni utaratibu wake wa kila siku kwenda kunywa pombe kisha kuanza kuleta vurugu hapa.

“Kwa hiyo, inawezekana alipigwa na wale watu aliokuwa akinywa nao pombe,” alisema mwanafunzi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles