32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel Money yaingia ubia na NMB

Airtel money rehcarge offerNa Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Airtel, Sunil Colaso, alisema: “Tunachofanya Airtel na benki ya NMB ni mwendelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika na nafuu.

“Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja wengi.

“Tunajisikia fahari kuona benki ya NMB inakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhahiri kwamba huduma za kifedha kwa mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa huduma kwa lengo la  kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika kufanya malipo,” alisema.

Alisema NMB itahudumia wakala wa Airtel zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima.

NMB na Airtel inaingia ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money.

Airtel Money imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na masharti magumu ya Timiza ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles