28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Yanga yampa mkono wa kwaheri Maximo

Marcio Maximo
Kocha mpya wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Marcio Maximo

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusufu Manji, amempa mkono wa kwaheri aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Marcio Maximo na msaidizi wake, Leonard Neiva na kumkabidhi rasmi madaraka kocha Hans van Pluijm na msaidizi wake, Boniface Mkwasa kukifundisha kikosi hicho.
Licha ya kuwaaga makocha hao, Manji hakuweka wazi sababu zilizowafanya kuwaondoa makocha hao zaidi aliwatakia kila la kheri huko waendako na kuwashukuru kwa ushirikiana wao.
Akizungumza kwa niaba ya Manji, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema sambamba na kufanya mabadiliko hayo ya makocha pia amependekeza sekretarieti mpya ya klabu hiyo ambapo Katibu Mkuu atakuwa Jonas Tiboroha, Mkuu wa Idara ya Masoko ni Omar Kaya huku Frank Chacha akiteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Sheria na Baraka Deusdeti kuwa Mkuu wa Idara ya Fedha.
“Mwenyekiti anapenda kuwashukuru makocha hao kwa kuwa pamoja kwa miezi sita kukinoa kikosi cha Yanga, lakini pia anaushukuru uongozi mzima uliomaliza muda wake,” alisema Muro.
Alisema Manji amewataka kufanya haraka makabidhiano ya ofisi zao ili kuwapisha viongozi hao walioteuliwa ili waanze kazi mara moja.
Maximo na msaidizi wake walianza kuwa katika wakati mgumu baada ya Yanga kufungwa mabao 2-0 na Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe wiki
iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles