33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji 10 kuwania uchezaji bora Ulaya

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

BERN, SWITZERLAND

NYOTA 10 wa soka kutoka klabu mbalimbali barani Ulaya wametajwa kuwania uchezaji bora wa mwaka mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.

Uongozi wa michezo barani Ulaya umeyataja majina 10 ya wachezaji waliotoa mchango kwenye timu zao kuwania tuzo hiyo, huku mshambuliaji wa klabu ya Wigan Athletic na timu ya taifa ya Ireland Kaskazini, Will Grigg, akiachwa kwenye kikosi hicho.

Awali mchezaji huyo alitajwa katika kikosi cha wachezaji bora 25 waliokuwa kwenye orodha hiyo ya wachezaji bora.

Hata hivyo, mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amepewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na mchango wake ndani ya klabu na timu ya taifa.

Mchezaji huyo amefanikiwa kutwaa Klabu Bingwa Ulaya huku akifunga bao la mwisho katika fainali dhidi ya Atletico Madrid, pamoja na kuifikisha Ureno fainali ya michuano ya Euro 2016 na kuchukua ubingwa dhidi ya Ufaransa.

Nyota mwingine ambaye anaonekana kuwa na nafasi kubwa ni mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, ambaye aliipeleka timu hiyo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, pamoja na kuifikisha timu ya Taifa ya Ufaransa katika fainali ya Euro 2016.

Griezmann alimaliza michuano ya Euro huku akiibuka mfungaji bora ambapo alifunga mabao sita, lakini anaonekana kuwa na ushindani na wachezaji wengine kama vila Gareth Bale wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales pamoja na mshindi wa msimu uliopita, Lionel Messi.

Riyad Mahrez, Jamie Vardy na N’Golo Kante ambao waliipa ubingwa wa ligi kuu klabu yao ya Leicester City, wameshindwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha watu 10, lakini walipata nafasi katika 20 bora.

Wachezaji hao 10 ambao wanawania tuzo hiyo ni pamoja na Gareth Bale wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gianluigi Buffon wa Juventus na timu ya taifa ya Italy, Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na timu ya France, pamoja na Toni Kroos wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujermany.

Wengine ni Lionel Messi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Thomas Muller wa Bayern Munich na Ujerumani, Manuel Neuer wa Bayern Munich na Ujerumani, Kepler Ferreira ‘Pepe’, wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Ureno pamoja na Luis Suarez wa Barcelona na Uruguay.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles