29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Joh Makini amkubali Paul Makonda

Joh Makini
Joh Makini

Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

MSANII wa muziki wa hip pop hapa nchini, Joh Makini, amekiri kuanza kumwelewa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, juu ya matatizo ya vijana kutokuwa na ajira.

Makini alisema hayo jana wakati akitambulisha wimbo mpya wa Perfect Combo, aliofanya na msanii kutoka nchini Nigeria.

“Kuna dhana tofauti sana juu ya kauli anazotoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya kufuata sheria na kuheshimu misingi ya katiba iliyowekwa, hivyo hapa hakuna kipya ila kinachotakiwa ni watu tuishi katika mstari ili tuweze kusonga mbele,” alisema Makini.

Makini aliongeza kuwa mbali ya  Makonda kuwa kiongozi pia ana maono ya mbali juu ya kizazi cha kesho katika mji unaoendelea kwa kasi kama Dar es Salaam.

Msanii huyo alitoa wito kwa wasanii na wadau wengine wa muziki kuendelea kumuunga mkono mkuu huyo wa mkoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles