27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jiji la Lagos kufunga misikiti, makanisa

Adebola Shabi
Adebola Shabi

LAGOS, NIGERIA

JIJI kubwa barani Afrika, Lagos, limetangaza kuwa litafunga baadhi ya misikiti, makanisa na vilabu vya usiku ili kupunguza kelele zinazowaathiri wakazi milioni 20 wa jiji hilo.

Serikali ya jimbo la Lagos, ilisema hatua hiyo itafanya jiji hilo lililo pwani ya Nigeria kutochafuliwa na kelele kufikia MWAKA 2020.

“Ni tatizo kubwa katika jiji hili,” alisema Adebola Shabi, mkurugenzi mkuu wa shirika la kutunza mazingira la Lagos.

“Tafiti zimeonyesha kwamba viwango vya juu vya kelele vinachangia uhalifu, ghasia na kuathiri afya zetu,” alisema.

Shirika hilo limefunga zaidi ya makanisa 70 na misikiti 20, vilabu na mikahawa mwaka huu.

Maafisa wakipokea malalamiko kutoka kwa wakazi, kuhusu kiwango cha kelele kinachotakiwa na iwapo kitazidi, serikali huchukua hatua na kufunga klabu, kanisa au baa ambako kelele hiyo hutoka.

Hata hivyo, watu wengi huogopa kulalamika. “Kuna kanisa na msikiti katika barabara ninayoishi na ni kama zinashindana nani anatoa sauti ya juu,” Charlie Chukwu aliambia shirika la habari ya AP.

“Waislamu waliponunua kipaza sauti kidogo, Wakristo walinunua kikubwa,” akaeleza.

Wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan uliomalizika mapema mwezi huu, alikuwa akiamshwa saa tisa usiku na wito wa Waislamu kwenda kusali kiasi cha kumkosesha usingizi, hali ambayo ipo kwa Wakristo wakiimba kanisani.

Chukwu alisema hakuwasilisha malalamiko yake kwa maafisa wa serikali. “ Ukiwaita maafisa wa serikali, basi unachukuliwa kwamba unapinga Ukristo, au Uislamu  na unakuwa adui wa wakazi mtaani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles