25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Unene wa kupita kiasi

BONGE

Utafiti wa mmoja kiafya duniani umeonyesha ongezeko la asilimia 82 la watu wanene kupita kiasi kati ya mwaka wa 1990 na 2010, likasema jarida la tiba la Uingereza, ‘The Lancet’, Volume 387, la Aprili 2, 2016

Vifo vinavyotokana na kunenepa kupita kiasi ni mara tatu zaidi ya vifo vinavyosababishwa na kukosa chakula chenye lishe, ingawa bado nchi nyingi zinapambana na ukosefu wa chakula.

Majid Ezzati, ambaye ni Profesa wa Afya ya Mazingira Duniani katika chuo cha Imperial cha London, Uingereza, alikuwa ni mmoja wa watafiti hao.

Ezzati alisema: “Katika ulimwengu ambao miaka 20 iliyopita haukuwa na chakula cha kutosha, sasa hivi tunapata magonjwa yanayotokana na kula kupita kiasi na vyakula vinavyoleta madhara, hata katika nchi zinazositawi.”

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Utafiti wa Kitaifa wa Afya na Lishe nchini Marekani (NHANES), uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wa Marekani ni wanene kupita kiasi, asilimia ambayo ni kubwa zaidi katika historia ya dunia. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa wanaume wanene kupita kiasi nchini humo ni asilimia 35.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles