32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mashirika ya kimataifa yaombwa kuhudumia wakimbizi

Kassim MajaliwaNa Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameyaomba mashirika ya kimataifa na nchi zilizoendelea zishirikiane na Serikali ya Tanzania katika kuwahudumia wakimbizi.

Aliyasema hayo   katika mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Dibr Reynders,   Dodoma jana.

“Kwa sasa tunashirikiana na Umoja wa Mataifa  kuwahudumia wakimbizi, hivyo tunaomba mataifa mengine nayo yatu-support  katika jambo hili,” alisema.

Alisema Tanzania  inahifadhi   wakimbizi 165,000 kati ya 230,000 walioko katika nchi za Maziwa Makuu, ambako bajeti ya Serikali haitoshelezi kuwapa huduma wanazostahili.

Waziri Mkuu  alisema wakimbizi hao wanaishi kwenye kambi mbalimbali nchini zikiwamo za Nyarugusu  na Nduta  wilayani Kasulu na Kibondo ambazo alizitembelea Desemba mwaka jana.

Alisema wakimbizi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za uhaba wa maji safi, ufinyu wa huduma za afya na elimu na uharibifu wa mazingira .

Aliwataja wakimbizi hao kuwa ni raia wa Burundi, Kongo na Rwanda.

Pia alimuomba  Reynders atakapofika Burundi akahamasishe amani.

Majaliwa alisema Tanzania inakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na mataifa mengine kuja kuwekeza katika sekta za viwanda, nishati na miundombinu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles