30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli afuta usajili wa hati shamba la mkonge

RAIS Dk. John MagufuliNa Amina Omari, MUHEZA

RAIS Dk. John Magufuli amelifuta kwenye usajili wa hati ya uwekezaji wa shamba la mkonge la Kibaranga  wilayani Muheza   lenye ukubwa wa hekta 5,730 lililokuwa limetelekezwa.

Akitangaza uamuzi huo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Kibaranga hapo jana, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema   rais amefikia uamuzi huo baada ya shamba hilo kutoendelezwa kwa kipindi kirefu.

Alisema kufutwa kwa shamba hilo na mengine ni hatua ya Serikali kuhakikisha inawapatia wananchi ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo badala ya kubaki mapori bila ya kuendelezwa.

Alisema kuwa moja ya ahadi ya Rais Magufuli ni kuhakikisha anafuta hati za mashamba yote yaliyomikiliwa na wawekezaji ambayo wameyakopea fedha benki bila ya kuyaendeleza na kuyarudisha serikalini kwa ajili ya kuyapangia utaratibu mpya ikiwamo kuwamilikisha wananchi ardhi hiyo.

“Serikali hii ya Rais Magufuli haina nia ya kuwakomoa wawekezaji kwa kuwanyang’anya mashamba bali tunataka tuwe na wawekezaji ambao wana malengo ya kuyaendeleza maeneo waliyochukuwa,” alisema Waziri Lukuvi.

Hata hivyo,   aliwataka wamiliki wa ardhi wengine ambao hawayaendelezi wayakabidhi serikalini wenyewe kabla ya Serikali haijayachukua maeneo hayo.

Wakati huo huo, aliagiza maeneo ambayo Serikali imeshachukua mashamba hayo, viongozi wa mkoa na wilaya wahakikishe wamewasilisha mpango wa matumizi bora ya ardhi hiyo katika  mwaka mmoja.

“Nawaelekeza viongozi wa wilaya na mkoa mhakikishe mnatengeneza utaratibu wa umiliki wa ardhi hiyo huku mkitoa kipaumbele kwa wananchi wanaoishi katika mashamba na si kujipa kipaumbele nyie viongozi,” alisisitiza Lukuvi.

Aliwataka kuandaa hati miliki ya ardhi kwa kila mwananchi  kuhakikisha Serikali inaongeza makusanyo yake kupitia kodi ya ardhi na wananchi wanapata fursa ya kupata mikopo kwenye taasisi za fedha kwa ajili ya maendeleo yao.

Alisema  utaratibu huo wa kutoa hati miliki utasaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina yya wananchi kwani watajua mipaka yao hivyo hakutakuwa na migogoro.

Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu aliipongeza Serikali kwa hatua yake ya kufuta hati ya umiliki wa shamba hilo ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika eneo hilo.

Alisema, shamba hilo lipo linapakana na vijiji viwili vya Kibaranga na Upare hivyo wananchi wake walikuwa hawana maeneo ya kulima kutokana na kuzungukwa na pori .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles