MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Ben Pol anayetamba na wimbo wake wa Moyo mashine, anatarajia kutoa burudani katika Tamasha la Nyama Choma litakalofanyika kesho katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.
Akizungumza jana, Mkuu wa Masuala ya Dijitali wa Tigo, Paulina Shao, alisema Tigo imekuwa ikiwapa moyo wasanii wa ndani ili kuhakikisha wanawezeshwa kufikia viwango vya juu katika kazi zao.
“Tigo inatambua mchango wa wasanii wa Tanzania wanaoutoa katika sekta ya burudani ndio maana tumewekeza kwa kiwango kikubwa kuwasaidia kwa kutumia majukwaa ya kidijitali yanayokuwepo na kushiriki matukio mbalimbali na hivyo kuongeza mauzo ya muziki wao pamoja na nembo zao,” alisema Shao.