Weusi, Isha Mashauzi kuzindua chandarua Mtwara

WeusiNA MWANDISHI WETU, MTWARA

WASANII Aisha Ramadhani maarufu Isha Mashauzi na kundi la muziki wa hip hop la Weusi, wanatarajiwa kushiriki kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria katika mradi unaojulikana kama Kliniki Chandarua.

Mradi huo unaotarajiwa kutoa vyandarua bure kwa mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa utazinduliwa kesho kutwa mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa mradi wa Victor Works, Noela Kisoka, amesema wasanii hao huhamasisha kampeni hiyo kwa kupitia muziki wao.

“Tunatarajia kuwa na wasanii kutoka Kundi la Weusi ambao wanaimba muziki wa kizazi kipya, lakini pia tutakuwa na mwanamuziki wa Taarabu, Isha Mashauzi ikiwa ni hatua ya kuufanya muziki kuwa sehemu ya hamasa ya utekelezaji wa mradi huu,” alisema Kisoka.

Mradi wa Kliniki Chandarua utazinduliwa mkoani Mtwara na mkuu wa mkoa, Halima Dendego, unatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali la Tanzania, Shirika la Victor Works na umedhaminiwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here