Na Amon Mtega, Songea
HALI za askari polisi watatu waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, baada ya kujeruhiwa na bomu lililotengenezwa kienyeji imeelezwa kuwa ni mbaya.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mungulu alisema jopo la madaktari linaendelea kutoa matababu kwa askari hao.
Aliwataja askari ambao hali zao si nzuri kuwa ni kuwa G7351 PC Ramadhan ,WP 10399 PC Felista wakati H 3484 PC Respicus ametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
MKURUGENZI wa upelelezi wa Makosa ya Jina nchini CP Issaya Mngulu amethibitisha kuwa Bomu waliotupiwa Askari polisi wannewaliokuwa wanne limetengenezwa kienyeji na kwa kitaalam zaidi kuliko mambomu mengine yaliyotengenezwa kienyeji ambayo yaliyowahi kulipuriwa katika maeneo mengine nchini ambapo hadi sasa hakuna mtu aliyeshikiliwa.
Alisema askari hao walikuwa wakifanya doria katika eneo la Mfaranyaki kuelekea Matalawe, lakini walipofika mtaa wa Mabatini karibu na nyumba ya kulala wageni ya Maliatabu kata ya Misufini ghafla walisikia kishindo kizito kikitua mbele yao.
Alisema msako mkali unaendelea ili kubaini watu waliohusika na tukio wanatakiwa mbaroni.
“Ndugu waandishi hawa waliofanya tukio ili tunaamini ni sehemu ya jamii tunayoishi nayo na mtu aliyetengeneza bomi hili ni lazima kuna mtu au watu waliomshuhudia au wanaomjua… kwa maana hakuwa peke yake, tunaomba wananchi watupatie ushirikiano.
“Nimekagua matukio mengi nchini yanayohusiana na milipuko ya mabomu, lakini tukio la Songea ni la aina yake.
Bomu linaonekana linakava ya bati gumu ambalo linaonyesha limetengenezwa kiufundi zaidi ,”alisema Mngulu.
Wakati huo huo, majeruhi wawili walioumizwa katika tukio hilo, wamesema hali zao zinaendelea vizuri na tayari wameshafanyiwa upasuaji. Akizungumza na waandishi wa habari wodi hapo,PC Ramadhan alisema alifanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia na kuondolewa masalia ya vibati viwili.
Alisema pia amepata michubuko sehemu za mgongoni na tumboni ambako kumetobolewa na kitu chenye ncha kali. Naye WP Felista, alisema bado anasumbuliwa na mguu wa kulia, ingawa ameanza kupata nafuu. Hata hivyo, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk.Benedicto Ngaiza alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.
Alisema WP Felista ameumia zaidi kwenye mguu wa kulia kutokana na kuvunjika mifupa mmoja. Tukio la askari hao, lilitokea juzi wakati watu wasiojulikana walipowarushia kitu kinachosadikuwa kuwa bomu na kuwajeruhi vibaya.Hadi jana hali kuna ambaye alikuwa amekamatwa. Mwisho