33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

TLP yawaomba Watanzania kuwaunga mkono kwa kuwapigia kura wagombea wao

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Chama cha Tanzania Labour (TLP) kimewaomba wananchi kuwaunga mkono katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwachagua wagombea wake kwa kuwa ni mahiri.

Akizungumza Novemba 23,2024 wakati wa kampeni zilizofanyika Mtaa wa Kwa Tumbo Kinondoni jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo, amesema wamedhamiria kuhakikisha mitaa mingi inachukuliwa na chama hicho na kuwataka wananchi kuwaunga mkono.

“Hatuna ruzuku lakini kwa kutumia wagombea wenyewe na wananchi wa maeneo husika tumefanikiwa kufanya kampeni zetu vizuri na tunafika maeneo husika na kuzungumza na wananchi. Tunaamini kutokana na wagombea tuliowaweka ambao tunaamini ni mahiri watakwenda kuchaguliwa kuwa viongozi katika maeneo yao,” amesema Lyimo.

Naye Mgombea Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwa Tumbo, Reuben Mmaje, amesema endapo atachaguliwa atahakikisha amani inakuwepo mtaani kwake wakati wote kwa kuwa hicho ni kipaumbele chake cha kwanza.

Aidha amesema atashughulikia changamoto ya masuala ya taka na ulinzi na kila nyumba itatozwa Sh 3,000 badala ya utaratibu wa sasa ambapo ada hiyo hutozwa kwa kila chumba.

“Vipaumbele vyangu vikubwa ambavyo ninavyo kwanza ni amani, nitahakikisha amani mtaani inakuwepo wakati wote. Tuna changamoto ya masuala ya taka na ulinzi; kila nyumba nitatoza Sh 3,000 ambayo itajumuisha pia na ada ya ulinzi.

“Mtaa wangu una nyumba 5,900 kwahiyo nimepiga hesabu nikaona nyumba 5,000 zinatosha kabisa kukidhi masuala ya ulinzi na taka, hizi zinazobaki 900 tunaacha kwa ajili ya wazee, wajane na wasiojiweza…habari ya mpango wa zamani wa kila chumba kuchangia Sh 3,000 haitakuwepo na huduma zote za kijamii zitatolewa bure hatutamtoza mwananchi,” amesema Mmaje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles