27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ushindi wa CCM unatokana na imani ya wananchi kwa kazi nzuri -CPA MAKALLA

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema CCM haihitaji kubebwa kwani inabebwa na kuuzwa na kazi nzuri zinavyofanywa na madiwani, Wabunge na Rais Samia Suluhu Hassan.

Makalla amesema hayo leo Novemba 24,2024 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ukonga Wilaya ya Ilala Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

“CCM inabebwa na kazi nzuri zinazofanywa na wabunge na madiwani wake, hivyo tunaimani CCM inauzwa na kazi nzuri iliyofanywa na waheshimiwa wabunge, madiwani na Mheshimiwa Rais, kwani kazi zake zinaonekana,” amesema CPA Makalla.

Sambamba na hayo, Makalla amesema CCM wanatembea kifua mbele kwa ajili ya kiongozi wao ambaye ni mwenyekiti kitaifa Rais Samia Suluhu Hassan na 4R zake na fedha anazozitoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Akizungumzia maendeleo yaliyofanywa na serikali ya CCM katika jimbo hilo amesema maji safi ya bomba yalikuwa ni historia na hadithi za kusadikika kwa wananchi wa eneo hilo lakini mbunge wao kupitia tiketi ya CCM, Jerry Silaa aliwapigania kuhakiisha wanapata miradi ya maji safi.

Makalla ameongeza akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alipata nafasi ya kusimamia ujenzi wa madarasa ya UVIKO na katika jimbo la Ukonga walipata bahati ya kupewa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mengi zaidi kuliko majimbo yote.

Pia amesema mbali na elimu na maji kuna maendeleo makubwa katika sekta ya afya kwa ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya katika kata mbalimbali na ujenzi wa mradi wa DMDP.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles