25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe apongeza kazi nzuri za ASA Nzega

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb) ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa shamba la mbegu Septemba 16, 2024 lililopo Undomo, Wilaya ya Nzega.

Shamba hilo lina ukubwa wa hekta 802.47 ambapo hekta 602 zimetumika kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu kwa kutumia mashine nne za pivot za umwagiliaji.

Katika kuendeleza dhana ya Serikali ya kuwa na ushirikiano na Sekta Binafsi, Kaimu Mkurugenzi wa ASA, Leo Mavika amesema kuwa hekta 11,160 za mashamba ya ASA nchini zinatumika kwa ajili ya kilimo cha mbegu kati ya zaidi ya hekta 13000 za ASA.

Ameeleza kuwa ASA imeimarisha usimamizi wa kila shamba ili yawe yanajiendesha kwa kujitegemea ili mahitaji ya shamba yawe yanafika kwa wakati, ikiwa ni pamoja na mbolea ya msimu ujao. Mavika pia ameeleza kuwa Taasisi imepanga kujenga ghala, kuweka mashine ya kuchakata na kukaushia mbegu, kujenga nyumba nne za watumishi na kujenga ofisi.

Kwa upande wake, Waziri Bashe ameonesha kuridhishwa na kazi ya shamba la ASA la Undomo na kuelekeza kuwa Taasisi inunue mashine tatu za pivot za umwagiliaji ili kukidhi mahitaji ya shamba lililopandwa na kuhitaji umwagiliaji la hekta 220 badala ya hekta 145 ambazo mashine zilizopo zinamwagilia kwa sasa.

“Ningependa pia ufanyike ukaguzi wa uhalisia wa matumizi ya shamba ili kuwe na data husika kwa ajili ya kuendesha shamba kwa ufanisi zaidi. Aidha, eneo la hekta 120 zira Hazar kwa mkandarasi ili shamba lote hatimae lillimwe na kuongeza uzalishaji wa mbegu,” amesema Waziri Bashe.

Waziri Bashe anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Nzega, ambapo amekuwa pia Shinyanga na Simiyu kuanzia Septemba 11, 2024.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles