Na Malima Lubasha, Serengeti
Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Msingi Nyamihuru Kata ya Busawe, wametakiwa kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya watoto wao wanaosoma shuleni hapo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Kemirembe Lwota wakati alipozungumza na wan afunzi wa shule hiyo ambao walimweleza kuwa wanafunzi wengine hawapati chakula kutokana na wazazi kushindwa kutoa mchango wa chakula na kuwaeleza wanafunzi kufikisha taarifa hiyo kwa wazazi na walezi hao.
Amesema jambo hili halipendezi kuona wanafunzi wengine hawapati chakula shuleni eti kwa sababu wa meshindwa kuchangia gharama za chakula kwani wanafunzi asipopata chochote tumboni usikivu wa masomo unakuwa haupo utakuta wengine wakiwa wanasinzia tu.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Daniel S Francis aliagizwa na mkuu wa wilaya kuhakikisha kuwa hili linatekelezwa kwa wazazi na walezi kunatoa michango sitapenda kuona wala kusikia jambo hilo linafanyika katika shule hiyo.
“ Lishe shuleni kwa wanafunzi hivi sasa ni muhimu sana watoto wakipata uji au chakula cha mchana usikivu wa masomo unaongezeka hata kiwango cha ufauru asilimia kinapanda hivyo nataka walimu kuhaki sha mnasimamia hili kuwahimiza wote wazazi wanachangia chakula kwa watoto wao mwalimu mkuu na kupa jukumu hili,”amesisitiza mkuu wa wilaya huyo.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili taifa liweze kupata watalaamu mbali mbali na kuzingatia maelekezo mnayopewa na walimu wenu kwa kujiepusha na utoro.
Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Francis amesema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 626 ina upungufu wa vyumba 4 vya madarasa yaliyopo ni 6 madawati yapoya kutosha yaliyopo ni 207 ikiwa ni pamoja na upungufu nyumba za walimu.